BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
HADITHI ya straika wa Vital'O, Laudit Mavugo kujiunga na Simba imeanza kusikika tena ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, Karikoo jijini Dar es Salaam huku naye akikiri juu ya ujio wake msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa uongozi huo pia upo katika mpango wa kumrejesha kikosini mshambuliaji wao Emmanuel Okwi ambaye anakipiga nchini Denmark katika klabu ya  SonderjysjkE kushindwa kufanya vizuri kwenye  yake.

Imeelezwa kuwa tayari uongozi wa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza umefanya mazungumzo na viongozi wa Simba ambao wameonyesha nia ya kumnunua mchezaji wao huyo àmbaye ni raia wa Uganda.

Mavugo alizungumza na BOIPLUS ambapo aliweka wazi kwamba ''Ni kweli nitakuja Tanzania msimu ujao. Sasa hivi nitakuwa mchezaji huru na hakuna atakayeingilia uamuzi wangu, kuna mambo madogo tu ambayo yatabadilika katika mkataba wetu na Simba ambao nilisaini nao mwaka jana.


''Naamini muda ukifika hatuwezi kushindwana na Simba na nitakuja kufanya kazi kwasababu hii ndio kazi yangu, awali viongozi wangu ndio walizuia mpango wa mimi kuja Simba,'' alisema Mavugo.

Viongozi wa Vital'O walizuia dili la Mavugo kwa kuipandishia dau Simba kutoka dola 60,000 hadi dola 100,000 kwa madai kuwa ana mkataba na klabu yao.

Simba pia inadaiwa kuwa huenda ikamtema mshambuliaji wao Hamisi Kiiza ambaye ndiye kinara wa mabao kwenye ligi akiwa amefunga mabao 19 kwa madai kuwa na utovu wa nidhamu pia hana ushirikiano na wenzake.

Wachezaji wengine wa kigeni ambao wanatajwa kutokuwemo kwenye usajili wa msimu ujao ni Raphael Kiongera, Brian Majwegwa na Emiry Nimubona huku Juuko Murshud na Justice Majabvi wakiwa mguu ndani mguu nje ila bado Simba inawahitaji wachezaji hao wawili.

Post a Comment

 
Top