BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye leo alishuhudia mechi ya Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la  Mbeya ikiifunga Coastal Union bao 4-0.

Mechi hiyo imechezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku yakiiweka pabaya zaidi Wagosi wa Kaya ambao wanashika mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 19 pekee walizozipata kwenye mechi 25 walizocheza.

Nape alipewa zawadi ya Fulana na viongozi wa Mbeya City alipotembelea halmashauri hiyo kwa shughuli za kikazi na kuamua kuitinga uwanjani na baada ya viongozi wa Coastal kuona Waziri huyo katinga uzi wa City walimkomalia ili avae uzi wao wenye rangi nyekundu.

Nape hakuwa na hiana ndipo alipoamua kuchukuwa uzi wa Coastal Union na kuutupia begani jambo ambalo liliwafurahisha Coastal Union.

Post a Comment

 
Top