BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
UONGOZI wa timu ya Mbeya City umesema unasubiri ripoti ya mwalimu Kinnah Phiri kuona kama kunahitajika kuongeza ama kupunguza wachezaji katika msimu ujao.

Katibu mkuu wa timu hiyo Emanuel Kimbe alisema wanasubiri msimu uishe wapewe ripoti na mwalimu ili wajue wanaongeza wapi kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha msimu ujao ambacho kitatoa ushindani mkubwa.

"Bado tuna michezo minne kumaliza ligi kwahiyo kuhusu nani ataingia au atatoka muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi kwa sasa tunafikiria michezo yetu iliyobaki,"alisema Kimbe.

Aidha katibu huyo alisema kwa sasa timu ipo katika mazoezi ya kujiwinda na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Aprili 30 katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.

Mbeya City imeshindwa kuonesha makali yake ya msimu wake wa kwanza ambapo  walishika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu bara huku hadi sasa wakiwa katika nafasi ya 10 baada ya kucheza michezo 26 na kujikusanyia alama 30.

Post a Comment

 
Top