BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Marco Ngavenga, Mbeya
MBEYA City imezidi kuipeleka Coastal Union kaburini baada ya leo kuifunga bao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Kwa matokeo hayo, City imefikisha pointi 27 na kupanda mpaka nafasi ya tisa huku Coastal Union ikiendelea kuwa mkiani ikikusanya pointi 19 na imebakiza mechi tano pekee sawa na Mbeya City. 

Mbeya City ilianza kuona lango la wapinzani wao dakika ya tatu tu tangu mchezo huo uanze kupitia kwa mchezaji wao Salvatory Nkulula aliyemalizia mpira alioutema kipa wa Coastal Union, Benedictor Haule  uliopitwa kwa shuti kali na Haruna Shamte.

Nkukula aliwainua tena mwashabiki wa City kipindi cha pili ikiwa ni piga nikupige langoni mwa Coastal Union ambapo Joseph Mahundi aliupiga kwenda winga ya kulia na kumkuta Hamid Mohamed wa Coastal kabla haujamtoka Nkulula akamnyang'anya na kuutupia wavuni.

Beki Hassan Mwasapili aliongeza bao la tatu dakika ya 74 akipiga shuti kali akiwa nje ya eneo la hatari shuti ambalo lilimshinda kipa wa Coastal baada ya kupaa juu yake na kutinga nyavuni.

Dakika ya 87, Ditram Nchimbi aliifungia City bao la nne kwa kichwa baada ya kutanguliziwa mpira na Mwasapili ndipo kipa wa Coastal akapaisha mpira huo uliomkuta Nchimbi.

Coastal Union walionekana kuzidiwa uwezo na Mbeya City kwani walikuwa wanachezewa nusu uwanja ingawa City wlaikuwa na bahati ya kupata nafasi nyingi za kuingia kwenye eneo la wapinzani wao lakini mashuti yao yalikuwa dhaifu na kushindwa kuleta madhara.

Katika mechi nyingine Mwadui amelalala kwa bao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mechi iliyochezwa Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Post a Comment

 
Top