BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
NAHODHA wa timu ya Simba Mussa Hassani Mgosi amesema msimu huu wamejipanga kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuukosa kwa misimu mitatu mfululizo.

Mshambuliaji huyo mkongwe ambaye hapati nafasi sana kwenye kikosi cha kwanza ameiambia BOIPLUS kuwa uongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wamejipanga kuhakikisha kombe linatua msimbazi baada ya kusubiri kwa muda mrefu.

"Umefika wakati wa wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba kufurahia ubingwa ambao sisi tumeamua upatikane mwishoni mwa msimu huu," alisema Mgosi.

Simba ndio vinara wa ligi hiyo kwa sasa wakiwa na pointi 57 baada ya kucheza michezo 24 huku watani zao wa jadi Yanga wakiwa nafasi ya pili wakijikusanyia pointi 53 baada ya kushuka dimbani mara 22. Wana lambalamba Azam Fc wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 51.

Mara ya mwisho timu hiyo kutwaa ubingwa ilikuwa ni msimu wa 2011/2012.

Post a Comment

 
Top