BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
BEKI wa kati wa timu ya  Azam, Said Morad amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku yeye mwenyewe akiamini kuwa bado anao ubora wa kuwa chaguo la kwanza kutokana na kiwango chake kwa sasa.

Akizungumza na BOIPLUS, Morad alisema anashangaa kuona hapangwi kwenye kikosi cha kwanza licha uwezo mkubwa alionao.

"Sijui hata kwanini nawekwa benchi uwezo bado ninao, mazoezi nafanya lakini bado nakaa benchi, ila kocha ndiye mwamuzi wa nani acheze katika mechi gani," alisema Morad.

Kuhusu mustakabali wake ndani klabu ya  Azam, Morad alisema "Nasubiri ligi imalizike ndiyo nitajua naenda wapi ila kwa sasa siwezi kukwambia chochote."

Kocha wa timu hiyo Stewart Hall amekuwa akiwatumia Paschal Wawa na Agrey Morris kama walinzi wa kati na akikosekana mmoja wao nafasi yake huchukuliwa na David Mwantika au Erasto Nyoni huku Morad akiwa chaguo la nne.

Post a Comment

 
Top