BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar


MMEMSIKIA Simon Msuva? Yaani kwao sasa kila mechi ya Ligi Kuu Bara wanafanya ni mechi ya fainali ili waweze kutetea ubingwa huo.

Yanga imefikisha pointi 59 wakati Simba kabla ya mechi ya leo Jumapili jioni dhidi ya Toto Africans ya jijini Tanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa ilifikisha pointi 57 na kwamba kuzomewa kwake ni jambo la kawaida.

Jana Jumamosi, Msuva aliisaidia timu yake ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mechi yao ya kiporo iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Msuva alisema "Tunacheza mechi nne ngumu ndani ya siku 10 ni changamoto kwetu tunapambana na nia yetu ni kufanya vizuri katika michezo yetu,"

Mchezaji huyo ambaye amekuwa akizomewa na mashabiki mara kwa mara anapokosea alisema kelele hizo ndizo zinamfanya aongeze jitihada na kujituma zaidi.

"Kuzomewa kwa mchezaji si kitu cha ajabu inatokea mara nyingi ulimwenguni kote, walinizomea nilivyofunga wakashangilia kwahiyo sina tatizo na hilo," alisema Msuva .

Post a Comment

 
Top