BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Dar
BABA mzazi wa straika wa Mwadui Fc Jerryson Tegete, John Tegete amevunja ukimya wake juu ya kushuka kwa kiwango cha mwanaye huyo na kusema kuwa chanzo ni timu ya Yanga.

Akizungumza katika kipindi cha Sports Bar kinachorushwa kituo cha televisheni cha Clouds, Tegete alisema sababu pekee iliyompoteza Jerry ni kuathiriwa kisaikolojia na jinsi alivyoondoka Yanga hasa suala la kudhulumiwa pesa yake ya usajili ambayo hajalipwa hadi leo.

"Jerry alivurugwa na jinsi alivyoondoka Yanga, katoka timu kubwa na kwenda ndogo, aliathirika sana kisaikolojia, isingekuwa rahisi kubaki katika kiwango chake.

"Lakini pia ameondoka pale Yanga akiwa anadai zaidi Sh. 15 milioni, TFF ilishamaliza kesi hiyo kuwa alipwe, lakini hakuna kilichofanyika hadi leo hii," alisema Tegete.

Tegete ambaye ni kocha mkuu wa Toto Afticans ya Mwanza alifunguka zaidi na kusema kuwa alipanga mwanaye akitoka Makongo aende Mtibwa na si Yanga, kilichomfanya asiende Mtibwa ni kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo ambaye aliomba aendelee kuwepo jijini Dar es Salaam ili iwe rahisi kwake kumtengeneza.

Post a Comment

 
Top