BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Dar
WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye leo alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Uhuru 'Shamba la Bibi', lakini akashtuka kukuta wachina wakiwa wamefungua kiwanda cha kutengeneza milango.

Uwanja huo unaojengwa na kampuni ya kichina ya BCEG umekuwa ukisuasua kukabidhiwa kwa serikali hali iliyopelekea waziri Nape aamue kutembelea ili kujionea kazi zinavyoendelea.

Katika ziara hiyo Nape alikuta wachina hao wakiendesha kiwanda cha kutengeneza milango kikiwa kinaendelea kufanya kazi ndani ya uwanja huo ambapo inasemekana milango zaidi ya 200 huzalishwa kila siku.

Nape aliamuru kiwanda hicho kifungwe huku akizitaka mamlaka husika ziende uwanjani hapo kufanya uchunguzi na meneja ampelekee ripoti kesho asubuhi. Wakati huo huo akiahidi kusimamia maslahi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Katika ziara hiyo pia Nape ametoa siku 30 mfumo wa tiketi za kielektroniki kwenye Uwanja  wa Taifa uwe umekabidhiwa kwake huku pia ikiahidiwa kuwa uzio wa uwanja wa Uhuru utamalizika ifikapo Aprili 19.

Post a Comment

 
Top