BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma
MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa dansi mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo Ndandason Anawemo Cossovo 'Ndanda Cossovo' anazikwa hii leo jijini Dar es Salaam baada ya kufariki kwa kuugua ghafla wiki iliyopita.

Cossovo ambaye wadau wengi wa muziki wa dansi nchini walianza kumfahamu alipokuwa na Bendi ya FM Academia International ambayo iliiundwa na wasanii wengi wenye asili ya Congo akiwemo rais wa sasa wa bendi hiyo Nyoshi el Saadat mwishoni mwa miaka ya 90.

Nyota ya Cossovo iling'ara zaidi baada ya kuachana na FM Academia na kuanzisha bendi ya Stono Musica ambayo waliita  'Wajela jela original' na kutunga kibao cha JELA na kumpa umaarufu mkubwa nchini ambapo alitunga baada ya kutoka jela yeye na wenzake baada ya kufungwa kwa kufanya kazi nchini bila kuwa na vibali.

Nyimbo nyingine alizotambanazo ni pamoja na Binadamu, Chozi la mnyonge na nyingine nyingi huku zikichagizwa na staili ya ' Kidedea' mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Baadae aliondoka nchini nakwenda Marekani kwa ajili ya shughuli za muziki kabla ya kurejea miaka ya karibuni na kuunda kundi lililoitwa Watoto wa Tembo ambapo halikudumu kabla ya kubakia kama mwanamuziki wakujitegemea.

Waziri wa Habari Sanaa na Michezo Nape Nnauye Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo nchini Jean Pierre Mutamba watawaongoza waombolezaji kwenye mazishi ya nguli huyo wa muziki wa dansi nchini.

Post a Comment

 
Top