BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar


MSANII wa muziki wa dansi Ndanda Kosovo amefariki dunia leo asubuhi kwa maradhi ya vidonda vya tumbo.

Msanii huyo ambaye ni raia wa DR Congo amefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo kifo chake kimethibitishwa na gwiji wa muziki nchini Mzee King Kikii.

Msiba wa msanii huyo upo Kinondoni ambapo taratibu za mazishi zikiendelea kwani imeeleezwa kuwa wanasubiri tamko la familia ya msanii huyo ambayo ipo nchini Congo kama asafirishwe ama azikwe hapa hapa nchini.

Imeelezwa kuwa endapo ndugu wa Marehemu wataridhia kwamba ndugu yao azikwe hapa hapa basi mazishi yake yatasubiriwa hadi ndugu hao wafike.

Post a Comment

 
Top