BOIPLUS SPORTS BLOG

DROO ya nusu fainali ya kombe la EUROPA imemalizika huku ikishuhudiwa Shaktar Donetsk wakipangwa na Sevilla mechi ya kwanza ikipangwa kuchezwa nchini Ukraine.

Nusu fainali ya pili itakuwa kati ya Villarreal watakaowakaribisha Liverpool nchini Hispania kwenye mchezo wa kwanza.

Mechi za kwanza za nusu fainali zitachezwa Aprili 28 na kurudiana Mei 5. Fainali ya EUROPA itachezwa kwenye uwanja wa Jakob-Park, Basel Mei 18

Post a Comment

 
Top