BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KOCHA Mkuu wa Mbeya City, Kinnah Phiri amemwondoa kikosini beki wake Hamad Kibopile kwa kosa la utovu wa nidhamu na kumtaka arejee kikosi hapo msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Tayari Kibopile ambaye ni mtaalamu wa kurusha mipira ya amekosa mechi kadhaa ikiwemo ile ya Mgambo JKT ambayo timu hiyo ilishinda na kujiwekea mazingira mazuri yatakayowafanya wakwepe kushuka daraja endapo pia watashinda mechi zao zijazo.

Phiri amekiri kumwondoa mchezaji huyo ambaye ameichezea City kwa misimu mitatu mpaka sasa "Huwa sikubaliani na tabia za utovu wa nidhamu, hiyo ni kanuni na sheria yangu ya kwanza ninapokuwa kwenye timu, nataka kila mmoja aheshimu kazi na asiwe juu ya kiongozi wake.

"Nafikiri atakaporejea msimu ujao atakuwa amejifunza na hatarudia, maana hatuwezi pia kuendesha timu kwa mfumo huu, mchezaji akikosea huwa namuonya lakini ikishindikana baada ya kuonywa anaondolewa kama adhabu yake," alisema Phiri.

Akizungumzia mechi yao ijayo dhidi ya Mtibwa Sugar alisema "Nimeangalia msimamo wa ligi wapo kwenye nafasi nzuri na hiyo inaonyesha si timu mbaya ya kuibeza, ninachokifanya sasa ni kuwaandaa wachezaji wangu ili mechi hiyo tushinde."

Mbeya City wamefikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 26 na wamebakiza mechi nne ambapo mechi tatu watacheza nyumbani na moja ugenini.

Post a Comment

 
Top