BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MECHI ya Mbeya City na Mtibwa Sugar imempa mtihani mkubwa kocha wa City, Kinnah Phiri amesema kesho atashinda kwenye televisheni 'kuichabo'  Mtibwa Sugar ikicheza na Yanga katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mbeya City kwasasa inajiandaa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar itakayochezwa Uwanja wa Manungu wilayani Turiani mwishoni mwa mwezi, mechi ambayo inaonekana kuwa ngumu kwa City inayopambana kubaki kwenye ligi msimu ujao ingawa tayari imefikisha pointi 30 sawa na Ndanda FC ya Mtwara

 "Baada ya mechi yetu ya Tanga nilitoa mapumziko ya siku saba, vijana watarejea   Jumatatu tayari  wa mazoezi  kabla ya kuivaa Mtibwa, nina  imani siku saba  zitatosha  kuwaweka sawa kwa ajili ya mchezo huo, siifahamu Mtibwa ila nimeona kwenye msimamo ipo nafasi nzuri.

"Ratiba inaonyesha watacheza kesho ninaweza kufika kuwaona au nitatumia muda wote kuangalia mchezo wao kwenye televisheni, nataka kujua baadhi ya mambo muhimu ili nijiandae vizuri kwa ajili ya kupata ushindi," alisema Phiri.

Kocha huyo ambaye ni raia wa Malawi alisema kuwa wachezaji wake wamerudi kwenye kiwango kizuri baada ya kupata matokeo mazuri katika mechi zao zilizopita na kwamba anahitaji ushindi katika mechi.

"Tulianza  kucheza kwa mchezo wa kawaida sasa tumeongeza, tunacheza kwa kasi kubwa, wachezaji wanajiamini kwa kiwango kikubwa, tumefunga mabao matano bila kuruhusu kufungwa bao lolote, jambo hili ni uhakika tosha kuwa kikosi changu kipo imara kwenye ulinzi na pia kwenye ufungaji, tuko kwenye mipango mizito kuhusiana na mchezo ujao," alisema.

Post a Comment

 
Top