BOIPLUS SPORTS BLOG

Simba wanajiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam jumapili, hapa makipa wa timu hiyo Manyika Jr na Vicent Angban wakiwa mazoezini huko Zanzibar.

Simba imeshajikusanyia pointi 57 ikiizidi Azam kwa pointi mbili, mechi hiyo itatoa taswira ya nani kati ya Simba na Azam atakuwa mpinzani wa Yanga kwenye mbio za ubingwa.

Kama Simba itashinda itafufua upya matumaini yao ambayo yalififishwa na Toto Africans baada ya kufungwa bao 1-0 katika mchezo wao wa mwisho wa ligi

Kocha Jackson Mayanja anataka kuona kikosi hicho kinapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani na njia pekee iliyobaki kwao ni kubeba ubingwa wa Bara.

Kiungo Said Ndemla, mmoja kati ya nyota wa Simba waliokuzwa klabuni hapo.

Baada ya kutolewa kwenye michuano ya Shirikisho, Simba wamebaki na jukumu moja tu la kubeba ubingwa wa bara, je, kikosi hiki kitaweza kuibuka na ubingwa huo ili wapate nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa?Manyika Jr akichupa kudaka mpira katika mazoezi yanayoendelea kisiwani Unguja.

Post a Comment

 
Top