BOIPLUS SPORTS BLOG

KIKOSI cha watoto wa Jangwani, Yanga kimetua salama nchini Misri kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya nchini humo.

 Katika mchezo wa awali, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 hivyo Yanga inahitaji ushindi wowote au sare ya kuanzia mabao 2-2.

 Hizi hapa ni baadhi ya picha za kikosi hicho baada ya kuwasili nyumbani kwa mafarao

 Yanga ina kumbukumbu ya kushinda michezo miwili ugenini katika michuano hii. Mwanzo ikiwafunga Cercle de Joachim ya Mauritius bao 1-0 kabla haijaenda kuibamiza APR ya Rwanda mabao 2-1

Mchezo kati ya Yanga na Al Ahly utapigwa siku ya jumatano.

Post a Comment

 
Top