BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
BEKI kisiki wa Azam FC, Paschal Wawa raia wa Ivory Coast ataukosa mchezo wa marudiano wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Esperance utakaochezwa April 19 nchini Tunisia.

Wawa aliumia katika mechi zao zilizopita na hivyo anaendelea na matibabu ataunga na kiraka Shomari Kapombe ambaye tayari amerejea nchini kutoka Afrika Kusini alikokwenda kupimwa afya yake.

Kapombe anasumbuliwa na matatizo ya mfumo wa damu tatizo alilopata baada ya kutoka Chad na timu ya Taifa 'Taifa Stars' dhidi ya Chad atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu na atakosa mechi zote za Ligi Kuu Bara zilizobaki.

Azam wanaondoka usiku wa leo kuelekea Tunisia pamoja na wachezaji mahiri Farid Musa na Himid Mao waliotakiwa kwenda kwenye majaribio Ubelgiji na Denmark.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd alisema "Wawa atakosa mechi hiyo kwani anaendelea na matibabu hivyo mpaka daktari aruhusu hali yake atakapoona yupo vizuri,"

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam, Azam ilishinda bao 2-1 dhidi ya Waarabu hao.

Post a Comment

 
Top