BOIPLUS SPORTS BLOG

 Na Zainabu Rajabu, Dar
KOCHA wa Yanga, Hans van Pluijm amesema kuwa mfumo aliotumia wa kupiga pasi za haraka ndiyo uliopelekea kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Mechi hiyo ya kiporo cha Ligi Kuu Bara ilichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na hivyo kuifanya Yanga ifikishe pointi 53 nyuma ya Simba yenye pointi 57.

"Tungeweza kufunga magoli mengi kwakuwa tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga kwani wapinzani wetu walikuwa pungufu, kupiga pasi za haraka ndiko kumetusaidia kupata ushindi huo na nitayafanyia kazi mapungufu niliyoyaona," alisema Pluijm.

Kwa upande wa Kocha wa Kagera Sugar, Adolf Rishard alisema walikuwa wanahitaji pointi hata moja ila nidhamu ya wachezaji wake iliwaangusha na kukosa umakini kwa mabeki wa kati ndiko kuliwamaliza kabisa.

"Katika siku ambazo mabeki wangu wa kati wamecheza vibaya ni kwenye mechi hii lakini hatukati tamaa na michezo yetu mitatu ya mwisho tutachezea nyumbani kitu ambacho kitatupa faida," alisema Adolf.

Post a Comment

 
Top