BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar
MASHABIKI wa soka hasa wapinzani wa Yanga wanadai kuwa timu hiyo inabebwa ndio maana inapata matokeo mazuri ila kocha Hans Van Der Pluijm ameweka wazi kuwa wanapata matokeo katika mazingira magumu.

Pluijm alisema kitu pekee kinachowasaidia kupata matokeo hayo ni kujituma na kujiamini kwa wachezaji wake na si vinginevyo.

Kauli hiyo aliizungumza baada ya mechi yao na Mtibwa Sugar iliyochezwa jana Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kupata ushindi wa bao 1-0 ambao uliwapandisha kileleni wakifikisha pointi 59.

"Nashukuru tumepata ushindi uliotuweka kileleni, ni ushindi ambao tumeupata katika mazingira magumu kutokana na wapinzani wetu kukamia pindi wanapocheza na sisi, wachezaji wangu pia hawakuwa makini kwani tulikosa nafasi nyingi za wazi," alisema Pluijm.

Kwa upande wa kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime alisema "Wachezaji wake walicheza vizuri ila walikosa umakini katika safu ya ushambuliaji, tumefanya makosa ambayo Yanga wameyatumia kutufunga,"

Post a Comment

 
Top