BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma , Dar
UONGOZI wa klabu ya Ruvu Shooting umejipanga kukifanyia marekebisho kikosi chao kwa ajili ya mikikimikiki ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao.

Ruvu Shooting ambayo imerejea baada ya kushuka daraja msimu uliopita, imejidhatiti kuhakikisha inatoa ushindani mkubwa kwa timu itakazokutana nazo .

Msemaji wa maafande hao Masau Bwire  alisema wanatarajia kuongeza wachezaji katika baadhi ya nafasi ambazo zililegalega  ili kuondoa mapungufu yaliyojitokeza katika ligi daraja la kwanza Tanzania bara.


"Tumerejea kwenye ligi na tunakuja na kasi kubwa huku tukijua kuna ushindani mkubwa na tumejipanga kufanya makubwa ili tuwaoneshe watanzania kuwa tulishuka kwa bahati mbaya.

" Kila timu itakayokutana na Ruvu Shooting msimu ujao ijipange kweli kweli kwakua tumedhamiria kufanya makubwa," alisema Masau.

Masau pia alisema watatoa ratiba ya timu hiyo muda si mrefu kwa ajili ya maandalizi ya ligi ikiwemo kuingia kambini na kucheza mechi za kirafiki.

Post a Comment

 
Top