BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda

MTANZANIA Mbwana Samatta amezidi kutisha kwenye ligi kuu nchini Ubelgiji baada ya leo kuisaidia timu yake KRC Genk kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Zulte-Waregem.

Samatta ambaye alifunga bao moja katika mchezo uliopita, aliipatia Genk bao la kwanza katika dakika ya nane tu tangu mchezo uanze. 

Mlinzi wa Zulte, Marvin Baudry alijifunga katika dakika 15 hivyo kuipatia Genk bao la pili kabla straika Mbaye Leye haijapatia Zulte bao la kufutia machozi dakika 45 kwa mkwaju wa penati.

Hii ni mechi ya kwanza kwa Samatta kucheza dakika zote 90 tangu ajiunge na wabelgiji hao huku hili likiwa ni bao lake la nne katika ligi hiyo.

Genk wamefikisha alama  30 ikiwa katika nafasi ya nne kwenye hatua hiyo ya sita bora (Play Off I) ambayo inaongozwa na Club Brugge yenye alama 38.

Post a Comment

 
Top