BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu na Bakari Kagoma, Dar
TIMU ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 ' Serengeti Boys'  imeifunga timu ya vijana ya Misri bao 2- 1 katika mechi yao ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bao lao kwanza la Serengeti Boys yalifungwa na Cyprian Benedictor dakika ya 10 baada ya kuwapiga  hemba mabeki wa Misri.

Makocha wa timu zote walifanya mabadiliko ambapo Serengeti Boys walitoka Mustapha Yusuph, Cyprian Benedictor wakaingia Gadafy Ramadhani, Boko Selemani.

Egypt wao waliwatoa Walid Ataia, Ibrahim Hassan, Mohamed Elsayed, Mohamed Tolba pamoja na Shaddy Hamam, Diaa Waheed na kuwaingiza Mohammoud Hegaze, Mohamed Mohamed, Youesef Osama, Mostafa Elyas, Hassan Zakarya na Fares Tarek

Waheed aliipatia bao la kufutia machozi Misri dakika ya 86 ikiwa ni piga nikupige langoni mwa Serengeti Boys ambapo dakika ya 90 Serengeti waliongeza bao la pili kupitia kwa Ally Hussein akipokea pasi ya Gadafy Ramadhan.

Post a Comment

 
Top