BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Chamazi
TIMU ya Taifa ya vijana chini ya  miaka  20 'Serengeti Boys' leo imeendeleza umwamba wao katika mechi ya pili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Misri kwa kuifunga mabao 3-2.

Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Chamazi wakati katika mechi ya awali iliyochezwa wiki iliyopita Uwanja wa Taifa Serengeti Boys ilishinda mabao 2-1.

Timu hiyo inayofundishwa na Kocha Kim Poulsen na mzawa Bakari Shime ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1 ambayo yalifungwa na Ibrahim Abdallah aliyefunga mawili na Boko Seleman.

Kwa upande wa Misri mabao yao yalifungwa na Hanzem Farghaly pamoja na Ahmed Saad.

Mechi hizo kwa Serengeti Boys ni maandalizi yao ya michuano ya kimataifa ambayo itafanyika baadaye mwaka huu nchini India.

Post a Comment

 
Top