BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar
KIUNGO wa Toto Africans ya Mwanza, Abdallah Seseme ametoa siri ya ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya Simba kuwa ni kucheza kwa kujituma katika muda wote wa mchezo na wala hawakubahatisha.

Akizungumza baada ya kumalizika mchezo huo Seseme alisema walikuwa katika nafasi mbaya ya kushuka daraja lakini wamepigana na kuonesha jitihada hadi walipofika sasa.

"Tulichofanya sisi ni kucheza kwa bidii kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo, Simba wanapocheza na sisi wanajua wanakutana na timu ya aina gani, tunawasumbua sana, " alisema Seseme.

Aidha kiungo huyo alisema wanarejea nyumbani kujiandaa mchezo wao dhidi ya Stand United katika uwanja wa CCM Kirumba wikiendi ijayo.

" Nia yetu ni kumaliza nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kutoanza vizuri."alisema Seseme.

Seseme alikuwepo kwenye  cha Kikosi Simba B kilichobeba ubingwa wa michuano ya Super8 iliyodhaminiwa na BancABC mwaka 2012 huku timu hiyo ikiwa chini ya kocha Suleiman Matola.

Post a Comment

 
Top