BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi wetu
TIMU  ya Simba ya jijini Dar es Salaam imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin Club Championship, inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) itakayoanza kutumia vumbi Mei 22, 2016 nchini Sudan.

Mashindano ya klabu Kombe la Nile Basin huandailiwa na CECAFA kwa kushirikisha timu zilizoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kwa nchi wanachama wa CECAFA.

Bingwa michuano ya kombe hilo atajinyakulia zawadi ya dola 30,000, mshindi wa pili dola 20,000, huku mshindi wa tatu akipata kitita cha dola 10,000.

Nile Basin inashirikisha klabu kutoka katika nchi wanachama wa CECAFA ambazo ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania na Zanzibar.

Vitoria University kutoka Uganda ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo baada ya kuifunga AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika mwaka 2014.

Post a Comment

 
Top