BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa 'Taifa Stars', inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya 'Harambee Stars' mechi hiyo itachezwa Mei 29, jijini Nairobi.

TFF kwa kushirkiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki, utakaotumika kama sehemu za maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON, Juni 2017 fainali hizo zitafanyika nchini Gabon.

Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha mkuu, Charles Boniface Mkwasa kinatarajiwa kuingia kambini mwezi ujao, mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili Misri katika uwanja wa Taifa jijini Dra es Salaam Juni 04.
Post a Comment

 
Top