BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi, Dar

 Timu ya Al Ahly ya Misri imetua alfajiri ya leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) kwa ajili ya kupambana na Yanga.


 Mafarao hao waliamua kutua kama mabubu na kuwa wagumu kuongoea chochote na wanahabari wachache waliokuwepo uwanjani hapo.


 Maafisa wa benchi la ufundi la timu hiyo wanakuna vichwa kujiuliza wanatokaje kwa watoto wa Jangwani?


 Mchezo huo wa ligi ya mabingwa Afrika utapigwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

 Hawa ni baadhi ya nyota wa timu hiyo wakiingia ndani ya basi lao tayari kuelekea Hotelini


 Muda mwingi walionekana wakiwa 'busy' na mambo yao huku wengine wakipiga picha tu


Yanga ambayo imejichimbia kisiwani Pemba, inahitaji ushindi mnono hiyo jumamosi ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuwatoa waarabu hao ambao kwa kawaida ni wagumu wakiwa kwao.

Post a Comment

 
Top