BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi, Dar

Mfungaji wa bao pekee la Yanga kwenye kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly, Donald Ngoma alipowasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere mchana wa leo. Yanga iliondolewa baada ya kufungwa mabao 2-1

 Kiungo nyota wa mchezo huo Thaban Kamusoko, alifanikiwa kuwadhibiti waarabu katika eneo la kati na kuwapa wakati mgumu katika muda wote wa mchezo huo

 Juma Abdul......huyu ndiye aliyetoa pasi ya bao pekee la Yanga, amekuwa mchezaji muhimu sana katika kikosi hicho huku akishiriki katika upatikanaji wa mabao mengi

 Vicent Bossou akipongezwa na mashabiki. Hakueleweka mwanzo, lakini sasa wanayanga utawaambia nini juu huu 'mkoba'?.

 Kipa Ally Mustafa 'Barthez' alikuwa benchi akisubiri kumsaidia Deogratius Munishi 'Dida'

 Katika uwanja wa ndege kulikuwa na shamrashamra za kutosha, asilimia kubwa ya mashabiki wa Yanga na watanzania kwa ujumla waliridhishwa sana na uwezo ulioonyeshwa na timu hiyo huko Misri huku wakiitabiria kufika mbali kwenye kombe la Shikisho la soka Afrika

 Tambwe akihojiwa na waandishi wa habari huku akipongezwa 'kiaina'Kiungo Boubacar Issoufou 

Post a Comment

 
Top