BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda


WABABE wa jiji la Madrid, Atletico Madrid ya Hispania wameibamiza Barcelona mabao 2-0 katika mchezo wa ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa kwenye dimba la Vicente Calderon.

Atletico waliingia uwanjani kwa kasi kubwa na kuanza kulishambulia lango la Barca wakionyesha wazi wanahitaji bao moja tu ili kusonga mbele katika michuano hiyo.

Antoine Griezmann aliwapa faraja mashabiki wa Atletico baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza kwa kichwa akimalizia krosi ya Saul Niguez katika dakika ya 36 kabla hajatupia la pili lwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 88.

Kwa ushindi huo Atletico imefanikiwa kuingia hatua ya Nusu Fainali kwa jumla ya mabao 3-2 kwani katika mchezo wa awali uliopigwa Camp Nou, Barca walishinda mabao 2-1.

Huko nchini Ureno, Bayern munich iliyokuwa ugenini imeikomalia Benfica na kutokanayo suluhu hivyo kuiondosha kwa jumla ya mabao 3-2, katika mchezo wa awali Bayern ilishinda bao mona tu.

Mabao ya wenyeji yalifungwa na Raul Jimenez na Anderson Taliscaf katika za 27 na 76 wakati yale ya wageni yakifungwa na Artudo Vidal pamoja na Thomas Muller kwenye dakika za 38 na 52.

Post a Comment

 
Top