BOIPLUS SPORTS BLOG


MABAO mawili yaliyofungwa kipindi cha kwanza na Ricardo Rodrigues pamoja na Maxmillian Arnold wa Wolfsburg katika dakika za 18 na 25 yalitosha kuwazamisha mabingwa wa kihistoria wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, Real Madrid.

Wolfsburg licha ya kuwa katika uwanja wa nyumbani hawakutawala sana mchezo huo ila walifanikiwa kwenye mpango wao wa kupata mabao yanayowaweka mahali pazuri kuelekea mchezo wa marejeano utakaopigwa ndani ya dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid.

Huko nchini Ufaransa, PSG wakiwa nyumbani wamelazimishwa sare ya mabao 2-2 na Manchester City hivyo kuwapa kibarua kigumu cha kulazimika kuondoka na pointi zote tatu katika uwanja wa Etihad kwenye mchezo wa marudiano.

Mabao ya PSG yalifungwa na Zlatan Ibrahimovic na Adrien Rabiot huku yale ya City yakiwekwa nyavuni na Kelvin de Bruyne pamoja na Fernandinho.Post a Comment

 
Top