BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi, Dar
YANGA jana iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar. Haikuwa kazi rahisi, ushindi huo ulipatikana baada ya kushuhudiwa vita kadhaa.
 Vita iliyovutia zaidi ni ile kati ya straika wa Yanga Donald Ngoma na beki kinda wa Mtibwa Andrew Vicent.

 Kamera ya BOIPLUS iliwamulika nyota hao na haya ni baadhi ya matukio yaliyonaswa.

Licha ya umahiri wa Ngoma, hakufanikiwa kuziona nyavu za Mtibwa  hiyo jana. Mtibwa watapaswa kumshukuru sana Vicent kwavile alitimiza vilivyo jukumu alilopewa la kwenda 'jino kwa jino' na Ngoma.
Post a Comment

 
Top