BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Dar
WANACHAMA wa klabu ya Yanga tawi la Facebook ( YAFF) wanatarajia kufanya mkutano wao mkuu kesho katika ofisi za tawi hilo zilizopo Tabata bima jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BOIPLUS msemaji wa tawi hilo Mustafa Zayumba 'Mucky' alizitaja ajenda za mkutano huo kuwa ni Ripoti ya kamati ya utendaji pamoja na kamati ndogo mdogo, Uendeshaji wa tawi (mapato na matumizi pamoja na madeni), Maendeleo ya tawi kwa ujumla  pamoja na Mengineyo.

"Tunawaomba wanachama wote wahudhurie mkutano huo bila kukosa kwa ajili ya maendeleo ya tawi hilo na Yanga kwa ujumla, utaanza saa 8 kamili mchana," alisema Mucky.

Tawi la YAFF ni moja kati ya matawi kadhaa yaliyoanzia kwenye mitandao ya kijamii wakati kwa Simba kukiwa na tawi la Simba Damu Fans (SDF) na Azam Die Hard Fans kwa upande wa Azam Fc.

Post a Comment

 
Top