BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma

DROO ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya itafanyika jijini Zurich Uswis kesho saa saba mchana kwa saa za Afrika Mashariki huku miamba minne ya soka ikitarajiwa kuonyeshana kazi katika hatua hiyo ambapo wawili kati yao watacheza fainali katika uwanja wa Stadio Giuseppe Meazza Mei 28.

Miamba iliyofuzu katika hatua hiyo ni Real Madrid na Atletico Madrid za Hispania, Bayern Munich ya Ujerumani na Manchester City ya Uingereza ambayo ndiyo mara ya kwanza kufika hatua hiyo katika historia ya klabu .

Mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya Barcelona tayari imeshaondelewa katika mashindano na Atletico Madrid kwa faida ya goli la ugenini baada ya kushinda nyumbani magoli 2-1 kabla ya kulala ugenini kwa magoli 2-0 jana.

Hii itakuwa ni fainali ya nne ya klabu bingwa barani Ulaya kufanyika katika uwanja huo huku zilizotangulia zikifanyika mwaka 1965, 1870 na 2001.

Uwanja wa Stadio Giuseppe Meazza ambao unatumiwa na Inter Milan hubadilika jina na kuitwa San siro kama unatumiwa na Ac Milan na una uwezo wa kuingiza mashabiki 81,277.

Fainali ya mwisho iloyofanyika uwanjani hapo mwaka 2011 Bayern Munich iliichapa Valencia ya Hispania kwa penati 5-4 huku golikipa wa Bayern kipindi hicho Oliver Khan ndiye alikuwa mchezaji bora wa mechi.

Post a Comment

 
Top