BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar
KAMATI ya Mashindano ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), imeipa ushindi Yanga kutinga hatua ya fainali ya Kombe la FA na sasa watacheza na Azam.

Katika kikao hicho ambacho bado kinaendelea imeelezwa kuwa Coastal wamenyang'anywa ushindi huo na kupigwa faini ya Sh 2 milioni kwa kumfanyia fujo mwamuzi huku mwamuzi Abdallah Kambuzi akifungiwa mwaka mmoja na mwamuzi wa pembeni Charles Simon akiondolewa kwenye orodha ya waamuzi.

Yanga pia imetozwa faini ya Sh 500,000 kwa kukataa kuingia vyumbani wakati mchezaji wa Coastal, Adeyuni Saleh amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa kosa la kumpiga mwamuzi.

Post a Comment

 
Top