BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
BEKI wa kati wa mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya Yanga, Kelvin Yondani amesema wanaweza wakaitoa timu ya Al-Ahly kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Yondani ameyasema hayo muda mfupi  baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 kwa kufunga goli la ushindi kwa mkwaju wa penati dhidi ya Ndanda na kuongeza kuwa kikosi chao ni bora kwa sasa na wanaweza wakawatoa waarabu hao.

"Watu wengi hawatupi nafasi ya kuwatoa Al-Ahly na sisi tumejipanga kufanya vizuri kwani Yanga ya sasa ni tofauti na zilizopita kwahiyo nawaomba mashabiki waje kwa wingi Aprili 9 kushuhudia tukimchinja mwarabu," alisema Yondani.

Katika siku za hivi karibuni beki huyo kisiki amekuwa akiaminiwa katika upigaji wa penati baada ya timu kukumbwa na jinamizi la kukosa mikwaju hiyo katika michuano mbali mbali na kocha Hans Pluijm amempa jukumu hilo.

Klabu ya Yanga imekuwa ikishiriki michuano ya kimataifa kwa misimu minne mfululizo lakini imekuwa ikishindwa kufika mbali ndiyo maana mashabiki wengi hawaipi nafasi ya kufanya vizuri hasa baada ya kupangiwa na Al-Ahly.

Post a Comment

 
Top