BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
 
MSHAMBULIAJI wa JKT Ruvu, Abdulrahman Musa ameibuka Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Mei.

Katika kinganyiro hicho, Musa aliwapiku Donald Ngoma wa Yanga na Ali Nassoro wa Mgambo Shooting. Mwezi huu ulikuwa na raundi tatu ambapo Musa alicheza mechi zote tatu za timu yake na kufunga mabao manne.

Kwa kushinda tuzo hiyo ya Mei ambayo ni ya mwisho kwa msimu huu, Musa atazawadiwa kitita cha Sh 1milioni kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.

Washindi wengine wa tuzo hiyo ya mwezi kwa msimu huu wa 2015/2016 ambao mechi zake za mwisho zilichezwa Mei 22 mwaka ni Hamisi Kiiza wa Simba (Septemba), Elias Maguli wa Stand United (Oktoba), Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba), Shomari Kapombe wa Azam (Januari), Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari), Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar (Machi) na Juma Abdul wa Yanga (Aprili).

Post a Comment

 
Top