BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar
MSHAMBULIAJI tegemeo wa timu ya Simba Ibrahim Ajib ameanza mazoezi baada ya kutoonekana uwanjani kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria.

Ajib ambaye timu yake ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 58 ameiambia BOIPLUS kuwa kwa sasa yuko fiti na  amerejea kupambana ili kuisaidia kumaliza mechi zilizobaki kwa ushindi licha ya kuwa matumaini ya kunyakua ubingwa yamepungua baada ya kuachwa pointi 10 na Yanga.

"Nimeanza mazoezi toka juzi niko tayari kuitumikia timu yangu sasa, kikubwa ninachoomba ni wapenzi wetu waendelee kutuunga mkono ili tushinde mechi zilizosalia," alisema Ajib.

Mshambuliaji huyo amekuwa na mchango mkubwa katika timu yake baada ya kutengeneza maelewano mazuri na Mganda Hamis Kiiza ambaye ana mabao 19, goli moja nyuma ya Amissi Tambwe anayeongoza kwa mabao 20.

Ajib ni zao la timu ya vijana ya Simba iliyochukua ubingwa wa BancABC mwaka 2012 chini ya kocha Suleiman Matola.

Post a Comment

 
Top