BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Dar
WAKATI kikosi cha Simba kikichanja mbuga kuelekea mjini Songea kwa ajili ya mechi yake na Majimaji  mshambuliaji wa timu hiyo Ibrahim Ajib ameondoka leo asubuhi kuelekea nchini Afrika ya Kusini kufanya majaribio katika klabu ya Kaizer Chiefs.

Ajib ambaye jana alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa ligi kuu ambao Simba walipigwa bao 1-0 na Mwadui Fc, ameelekea nchini humo kufuatia mwaliko aliopata kutokana na kiwango cha hali ya juu alichoonyesha msimu huu.

Mshambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira atakuwepo nchini humo kwa muda wa wiki mbili kabla hajarejea nchini ambapo atakuta timu yake imeshamaliza ligi.

Kama atafuzu na kujiunga na vigogo hao, klabu ya Simba itaendeleza sifa yake ya kuuza wachezaji nje huku ikiwa ilishawauza wachezaji kama Mbwana Samatta, Patrick Ochang (TP Mazembe), Henry Joseph (Kongsvinger Fc), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya), Emmanuel Okwi (Sonderjyske) na wengine kadhaa.

Habari za ndani zinasema mkataba wa mchezaji huyo na Simba unaelekea ukingoni ingawa viongozi wake waliwahi kunukuliwa kuwa ana mkataba wa mwaka mmoja mbele.

Post a Comment

 
Top