BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Bakari Kagoma, Dar
MFUNGAJI bora wa michuano ya kombe la FA iliyomalizika jana  Atupele Green ameweka wazi kuwa ligi ilikuwa ngumu na timu zilijipanga ila anamshukuru Mungu kwa kuibuka kinara kwenye upachikaji mabao.

Mshambuliaji huyo tegemeo wa Ndanda FC ambaye hakuwahi kupata tuzo yoyote katika historia yake ya mpira, alisema ni heshima kwake kuibuka mfungaji bora japokuwa anatokea kwenye timu ndogo ambayo ndiyo ina misimu miwili tangu ipande daraja.

"Hii ni tuzo yangu ya kwanza sijawahi kupata kabla, nawashukuru wachezaji wenzangu kwa mchango wao hadi leo hii nimeibuka kinara, bila wao isingewezekana," alisema Atupele.

Aidha Atupele alisema kuna uwezekano mkubwa msimu  ujao asiwatumikie 'Wana kuchele' hao baada ya timu mbali mbali zinazoshiriki ligi kuonesha nia ya kuhitaji huduma yake huku mkataba wake na Ndanda ukiwa ukingoni.

"Bado sijajua nitakuwa wapi msimu ujao kuna timu zimenifuata ila hatujafikia makubaliano yoyote katika upande wa maslahi.

"Timu yoyote itayokuja na tukakaa meza moja na kukubaliana maslahi yangu nitasaini hata waajiri wangu Ndanda wakitaka tuendelee kuwa pamoja niko tayari," alimalizia Atupele.

Atupele ni miongoni mwa washambuliaji wazawa waliofanya vyema msimu uliomalizika huku klabu kubwa nchini zikionesha nia ya kuhitaji huduma yake.

Post a Comment

 
Top