BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Nitike Ahazi, Dar
JAMBO pekee ambalo alikuwa akilitamani straika wa Ndanda FC, Atupele Green  kulifanya katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara ni kuzisumbua safu za ulinzi za Simba na Yanga ambapo ameweka wazi kuwa alifanikiwa kwa asilimia zote.

Akizungumza na BOIPLUS, Atupele alisema tayari amefanikiwa kuzifunga Simba na Azam, pia kuisumbua vilivyo ngome ya 
Yanga na kuisababishia penati, ila alichobaini ni utofauti wa kipato tu na siyo kwamba wana uwezo wakutisha.

"Ukitaja jina la beki Pascal Wawa (Azam), Juuko Murshid (Simba) na Kelvin Yondan ( Yanga), unaweza ukaogopa kujituma lakini mimi niliweka dhamira kuhakikisha 
naonyesha uimara wangu," alisema Atupele.

Alisema aliamua kuthubutu kuwasumbua mabeki wa timu hizo tatu baada ya kuona 
straika wa Yanga, Donald Ngoma ana mwili kama wake na anaaminika kwa kusumbua mabeki wa timu pinzani timu yake inapocheza na wanafanikiwa kupata matokeo mazuri.

"Nimeamini kwamba kila kitu ni kujaribu na siyo kuogopa nimeona mafanikio yake 
kwani tayari nimeona jinsi ambavyo nimeweza kuwafuata na wao kunikaba kwa shida, 
ila tofauti ni kwamba timu zao ni tajiri sisi tunakumbwa na ukata," alisema.

Post a Comment

 
Top