BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar
UONGOZI wa Klabu ya Azam FC, unatarajia kutumia mechi ya fainali ya Kombe la FA kumuaga kiungo wao Farid Musa huku ikiweka wazi kuwa hawana  mpango wowote wa kumsajili mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu.

Farid amefuzu majaribio yake katika klabu ya Las Palmas ya Hispania  ambapo atarejea nchini kwa ajili ya kukamilisha makubaliano kati ya pande hizo mbili hivyo atacheza mechi ya fainali ya FA dhidi ya Mabingwa wa ligi, Yanga itakayochezwa mwezi ujao.

Ajib yeye yupo nchini Afrika Kusini ambako anafanya majaribio, amekuwa akitajwa kusakwa na Azam pamoja na Yanga huku ikielezwa kwamba mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu ila viongozi wake wamedai mkataba huo unamalizika mwakani.


Mkurugenzi Mtendaji wa Azam FC, Saad Kawemba amesema kuwa kuondoka kwa mchezaji wao huyo hakuwezi kuwaathiri lolote kwani wana vijana wengi wenye vipaji huku akimtolea mfano Mudathir Yahaya.

''Tuna wachezaji wengi wazuri ambao wanaweza kuziba nafasi ya Farid na hatuwezi kununua mchezaji anayetoka kwenye  Ligi Kuu hapa nchini, huyo Ajib (Ibrahim) si mchezaji wa kucheza Azam, watu kama wanataka kumnunua wampe thamani yake na siyo kumuunganisha na Azam ili aonekane ana thamani kubwa ili watu watoe pesa  nyingi.''

Post a Comment

 
Top