BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
BENCHI la Ufundi la Azam Fc litaondoka baada ya mechi yao ya mwisho dhidi ya Mgambo JKT itakayochezwa Mei 21 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Kocha wa Azam, Stewart Hall amethibitisha hilo na kwamba ameona ni vyema aondoke ili kocha mwingine ajaribu kufanya mabadiliko kwani tangu atue Tanzania hajaona mabadiliko yoyote kwenye soka.Hall ataondoka pamoja Mario Marineca wa England na Mromania, Adrian Dobre ambaye ni mtaalamu wa viungo.

Hall aliwahi kuifundisha Azam mwaka 2010 kwa mafanikio makubwa ingawa baadaye aliondoka na kumwajiri kocha Joseph Omog aliyetimuliwa siku chache tu Azam ilipoondolewa kwenye michuano ya kimataifa mwaka juzi ndipo Hall alirejeshwa tena.

Ingawa Azam imekuwa ikishiriki michuano ya kimataifa lakini bado mwenendo wake si mzuri sana japokuwa inapata mahitaji yote na ndiyo timu tajiri kwenye Ligi Kuu Bara huku wakiwa na wachezaji bora wanaolipwa mishahara minono.

"Sioni sababu ya kuendelea kuifundisha Azam wakati hakuna mabadiliko yoyote tangu miaka ya nyuma, hivyo nitaondoka baada ya mechi ya Mgambo na timu ataachiwa kocha msaidizi, Kitambi (Denis) lakini pia wengine wote wa benchi la ufundi wataondoka," alisema Hall.

Hall hataisimamia Azam kwenye mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Yanga itakayochezwa mwezi ujao.

Post a Comment

 
Top