BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Bakari Kagoma, Dar
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania TFF na Azam TV zimesaini mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya bilioni mbili kwa ajili ya kudhamini ligi ya wanawake na vijana chini ya umri wa miaka 20.

Ligi ya wanawake ambayo itaanza Agosti mwaka huu itashirikisha timu 10 ambazo zitatoka katika mikoa ambayo tayari ilishacheza ligi msimu uliopita.

Rais wa shirikisho hilo Jamal Malinzi aliupongeza uongozi wa Azam Media kwa kuwekeza katika soka la wanawake na vijana ambalo lilitelekezwa kwa muda mrefu na kuyaomba makampuni mbali mbali kujitokeza kusaidia soka la akina mama.

"Naishukuru Azam Media kwa kujitokeza kusaidia soka la wanawake ambalo litasaidia kupata timu bora ya taifa, Twiga stars," alisema Malinzi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Azam Media, Rhy Tomngton alisema wataendelea kuwekeza katika soka la Tanzania ili kulitangaza kimataifa.

Naye Mwenyekiti wa soka la wanawake Tanzania Amina Karuma alisema Azam Media wameonesha njia ambayo itakuwa ni msaada mkubwa kwa soka la wanawake ambalo limekuwa likikosa udhamini kwa miaka mingi.

Post a Comment

 
Top