BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
AZAM FC leo imeifunga Kagera Sugar mabao 2-1 matokeo ambayo ni mabaya kwa Kagera Sugar kwani yanazidi kuwadidimisha kwenye hatari ya kushuka daraja. Mechi hiyo imechezwa Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Kagera inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 25 huku ikibakiwa na mechi tatu pekee ambazo wanatakiwa kushinda ili wabaki kwenye ligi msimu ujao na kama watapoteza basi nao watakuwa wamejiondoa ushiriki wao wa msimu ujao.

Mabao ya Azam ambayo yaliipa pointi tatu na kupanda nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 60 yalifungwa na Himid Mao pamoja na Kipre Tchetche huku bao la Kagera likifungwa na Adam Kingwande.

Katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Prison waliikaribisha Majimaji ambayo ilikubali kipigo cha bao 2-0. Mabao ya Prisons yalifungwa na Jeremiah Juma na Adam Chimbongwe.

Pamoja na kupoteza mechi hiyo, Majimaji wanabaki kwenye ligi kwani wana pointi 33 sawa na Mbeya City pamoja na Ndanda ambazo zote zina mechi mkononi. Prisons yenyewe imefikisha pointi 45.

Post a Comment

 
Top