BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Chamazi
TIMU ya Azam FC ni kama vile imekubali matokeo kuwa haitochukua   ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu baada ya kulazimishwa sare ya magoli 2-2 na maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Chamazi Complex.

Mechi hiyo ilianza taratibu huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini walikuwa ni Azam ambao walipata goli la kwanza dakika ya 31 kupitia kwa Michael Bolou baada ya kumalizia krosi ya Mudathir Yahaya na dakika tano baadae Kipre Tchetche alifunga goli la pili kutokana na pasi mzuri ya Himid Mao.

Kipindi cha pili JKT Ruvu walionekana kubadilika baada ya kumuingiza Samwel Kamuntu na kufanikiwa kupata goli kwa mkwaju wa penati dakika ya 56 lililofungwa na Saad Kipanga baada ya beki Gadiel Michael kuushika mpira katika eneo la hatari.


JKT waliendelea kulisakama lango la Azam na dakika ya 72 Musa Juma aliwapatia maafande hao goli la kusawazisha baada ya mabeki wa wana lamba lamba kushindwa kuondoa mpira katika hatari.

Azam waliwatoa David Mwantika,Mudathir Yahaya Michael Bolou nafasi zao zikachukuliwa na Said Morad, Ramadhani Singano  Mcha Hamisi huku JKT Ruvu wakipumzisha Abdulahman Musa, Musa Juma na kuwaingiza Samwel Kamuntu na George Minja.

Azam wamefikisha alama 60 na kuwa nyuma kwa alama 8 dhidi ya vinara Yanga huku wakiwazidi Simba walio nafasi ya tatu kwa pointi 2. Yanga sasa wanahitaji alama tatu tu ili watangaze Ubingwa kwavile hakuna timu inayoweza kufikisha alama 71.

Post a Comment

 
Top