BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
KLABU ya Azam FC leo imeingia mkataba wa miaka miwili kwa makocha wao wapya, Zeben Hernandez raia wa Hispania pamoja na kocha wa viungoJonas Garcia huku Denis Kitambi akiendelea na ajira yake ya kocha msaidizi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa klabu hiyo, Jaffar Idd alisema kuwa mikataba wa makocha hao itaanza rasmi msimu ujao ambapo tayari kocha wao mkuu, Stewart Hall na wenzake wameishaaga tayari.

Hata hivyo makocha hao wanaweza kuanza kuisimamia Azam kwenye mechi ya fainali ya Kombe la FA  dhidi ya Yanga itakayochezwa Mei 25 badala ya Juni 11 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

"Baada ya kutua nchini, viongozi waliendelea na mazungumzo kwa ajili ya makubaliano ya mkataba na sasa wamefikia muafaka ambapo wamesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu yetu lakini Kitambi atabaki kama kocha msaidizi na Garcia ni kocha wa viongozi," alisema Jaffar

Hall aliamua kuachana na Azam kwa kile alichodai kutokuwa na jipya ndani ya kikosi hicho tangu aanze kuifundisha kutokana na mfumo mbovu wa soka la Tanzania hivyo aliona ni vyema akawaachia wengine wajaribu kuitoa Azam hapo ilipo na kuipeleka hatua ya mbele zaidi.

Post a Comment

 
Top