BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Nitike Ahazi, Dar
KOCHA wa timu ya Kagera Sugar, Adolf Rishard, ameweka wazi kwamba msimu huu ulikuwa wa machungu kwake kwani timu yake ilifanya vibaya ingawa matumaini yalirejea dakika za mwisho baada ya kikosi chake kunusurika kushuka daraja

Rishard aliiambia BOIPLUS kuwa: "Haikuwa kazi rahisi, kocha ukiwa na roho ndogo unaweza kukimbia timu lakini niliamua kupambana hadi kufanikisha kubakiza timu ,"

Rishard alisema ligi ya mwaka huu ilikuwa na changamoto nyingi ambazo wanapaswa kujipanga ili msimu ujao timu yao ipate matokeo mazuri kuanzia mechi za awali ikiwemo kufanya usajili wa maana.

"Safu yetu ya ushambuliaji ilionekana kuwa butu ni kati ya mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi kikamilifu kwani hatuhitaji kuendelea na kasumba ya kujinasua Kagera ni timu kongwe inayohitaji ushindani wa kutosha," alisema

Kocha huyo alisema anaandaa ripoti ya kuelekeza kinachotakiwa kufanyika ili viongozi waweze kujipanga mapema.

Post a Comment

 
Top