BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi,Dar
MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Yanga hawajafanya mazungumzo yoyote juu ya kumpa mkataba mpya kiungo wao Salum Telela ambapo mkataba wake unamalizika mwezi huu huku akitajwa kumwaga wino Simba.

Telela ameimbia BOIPLUS kuwa haelewi mustakabali wake ndani ya klabu hiyo baada ya viongozi kukaa kimya huku wakijua mkataba wake unamalizika.

"Mkataba wangu unamalizika mwishoni mwa mwezi huu lakini cha kushangaza hadi leo hakuna kiongozi yoyote alieniulizia kuhusu kuongeza mkataba,"alisema Telela

Alipoulizwa kuhusu kusaini mkataba na Simba alisema: "Sijasaini Simba wala timu yoyote ila muda ukifika kila kitu nitakiweka hadharani,"


Kwa wiki moja sasa kumekuwa na taarifa za kiungo huyo kujiunga na Simba ingawa mwenyewe ameukana uvumi huo.

Post a Comment

 
Top