BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Nitike Ahazi, Dar
NYOTA wa zamani wa Yanga, Said Bahanuzi ambaye kwa sasa anaitumikia Mtibwa Sugar, ameweka wazi kwamba klabu kongwe zina faida ya kutangaza vipaji vya wachezaji ila kwa upande mwingine zinafanya washindwe kuvuka mipaka ya nchi.

Bahanuzi alifafanua kwamba: "Ni kweli Simba na Yanga, ukizichezea unaweza kupiga hatua kimaisha lakini usipokuwa makini zinaweza kukufanya udharaulike mbele ya jamii 
kwani zinakandamiza wachezaji pamoja na kuwapumbaza ili wasiwaze mbali." 

Mwaka 2012, Bahanuzi ndiye alikuwa mfungaji bora wa Kombe la Kagame akiwa na 
Yanga, alisema klabu hizo hazina ushauri kwa mchezaji pindi anapokuwa anatazamwa 
na timu za nje badala yake zinajenga mazingira ya kufaidika wenyewe huku zikimwacha mchezaji akiwa masikini.

"Mchezaji hata aking'ara akiwa Yanga na Simba ni ngumu kiwango chake kufika mbali 
ataishia kushangiliwa na mashabiki mwisho wa siku akichoka ndiyo anaanza kusaka timu 
za nje ambazo hazina hadhi ili mradi tu aonekane amecheza soka la kulipwa," alisema Bahanuzi.

Alizungumzia juu ya wachezaji kutojielewa, alisema kwamba hiyo inatokana na uwepo wa  viongozi wa klabu ambao wana mifumo ya kukandamizi wachezaji.

Post a Comment

 
Top