BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
BAADA ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika kiungo fundi wa Yanga Haruna Niyonzima amefunguka kuwa malengo yao yametimia.

Yanga iliitoa timu ya Sagrada Esparanca ya Angola kwa jumla ya magoli 2-1 katika michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini na kwa  mara ya kwanza tangu 1998  mabingwa hao ndiyo wamefanikiwa kufika  hatua hiyo tena.

Niyonzima alisema haikuwa kazi rahisi kufika hapo, walipagana sana kuhakikisha wanawapa raha wapenzi na wanachama wa timu yao japokuwa Esparanca waliwafanyia matukio mengi yasiyo ya kiungwana.

"Ni fahari kwetu kufikia hatua hii, tulipambana sana haikuwa kazi rahisi tunapata mchango mkubwa toka kwa viongozi, wapenzi na wanachama hatimaye tumefikia malengo yetu," alisema Niyonzima.

Aidha Niyonzima ambaye ni raia wa Rwanda alisema bado wana kazi kubwa ya kupambana na vigogo wa soka barani Afrika waliofanikiwa kufika katika hatua hiyo.

Miongoni mwa timu zilizofuzu hatua hiyo ni pamoja na TP Mazembe, Etoile du Sahel, Madeama na Al Ahly Tripoli ya Libya.

Droo ya makundi inatarajiwa kufanyika Jumanne wiki ijayo.

Post a Comment

 
Top